Supastaa wa Kike wa muziki wa Bongo Flava, Rehema Chalamila a.k.a ‘Ray c’ au ‘Kiuno bila mfupa’, ameibuka na kuanika ukweli juu ya skendo yake y madai ya kutapeli nchini Swiden.
Akiongea kupitia mtandao wa Bongo5 Ray C alisema kuwa yeye hajamtapeli mtu yeyote na anashangaa uvumi huo kusambaa hadi kuandikwa katika vyombo vya habari kuwa ametapeli.
Alisema kuwa anajua anayetangaza mambo hayo ni mtu mmoja anayeitwa Hassan lakini si Promota wake kwani huyo bwana ndiye aliyetoa namba yake ya simu kwa mapromota wake ambao ni waganda kwa ajili ya kumtafuta shoo nchini Holland, Sweden na Norway.
Aliwataja waganda hao kuwa ni Eddy na Joachim na kusema kuwa ndio watu ambao alipatana nao kwenda kufanya shoo katika nchi hizo na walimuahidi wangemtumia nyaraka za mualiko wakiwa wamekamilisha kila kitu.
Aidha Ray C aliendelea kutiririka na kusema kuwa baada ya kumtumia nyaraka alienda nazo Ubalozini lakini alipofika huko aliambiwa kuwa hawezi kupewa viza kwasababu watu waliomualika walikuwa si raia wa Sweden.
“Mimi nashangaa watu wananitangazia kuwa nimetapeli, nimetembea nchi ngapi si chini ya arobaini nikifanya shoo, kwanini nisitapeli nije kutapeli leo? Ukweli ni kwamba natamani sana kuja Ulaya kwani Dar es salaam kuna joto sana na mambo yakikamilika nitakuja” alikaririwa Ray C.
“Unajua tatizo kubwa lilotokea ni wao maproduza kutangaza shoo kabla hawajakamilisha mipango ya viza kitendo ambacho kimenichafua na kuniharibia kwani walitakiwa kukamilisha mipango yote ndipo watangaze,” aliongeza Ray C.
Alisema kuwa kwa sasa amepata fundisho na kuwaomba watu wote wanaomuhitaji kuwa makini katika kukamilisha mipango yote ndipo wamtangazie shoo na kwamba siku nyingine hatakubali mtu kutangaza shoo zake kabloa ya kukamilisha mambo.
“Nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani mapromota wangu anakwenda sambamba kuhakikisha anakamilisha Document (nyaraka) zinazotakiwa, kisha nije kufanya shoo,” alisema Ray C.
No comments:
Post a Comment